Count Down
About Me
Saturday, September 17, 2016
Wednesday, July 27, 2016
BOLD , ITALIC & TILD ndani Ya WHATSAPP sasa
Jinsi ya kuweka Bold, tilde na Italic kwenye Whatsap
Watu wengi husumbuka sana wanapoandika ujumbe kwenye app ya WhatsApp kutokana na hali kwamba herufi huwa na uzito sawa wa rangi katika hali ya kawaida. Mtindo huwa mmoja tuu, ila kuna namna ya kufanya kuwa tofauti.
Whatsapp: Bold, Italic na Strikethrough
Je, wajua unaweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (Italic) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati (strikethrough) kwenye Whatsapp?
Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu yako.
Kuweka bold
Ili kukoza rangi kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na alama ya nyota na kisha kuhitimisha na alama ya hiyo hiyo ya nyota kwa mfano ukiandika bold itatokea ikiwa bold.
Whatsapp: Jinsi ya kufanya ili ujumbe wako uwe bolded
Kuweka Italic
Ili kufanya herufi zako kuwa za mlazo (italic), unahitajika
kutanguliza na mstari sakafu (underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo. Kwa mfano ukiandika “ italics” itatokea ikiwa Italics.
Jinsi ya kufanya ili ujumbe wako uwe katika mfumo wa Italics
Kuweka strikethrough(tide)
Ukitaka kuweka alama ya kukata kati kwenye herufi zako, unahitajika kuanza na alama ya mawimbi [tilde (~)] na kuhitimisha na alama iyo hiyo . Kwa mfano ukiandika “~strikethrough~” itatokea ikiwa na mstari uliokata herufi kati.
Ujumbe ukiwa katika mfumo wa strikethrough
Kuunganisha mitindo
Unaweza ukataka kuunganisha mitindo, mfano utake maandishi yako kuwa na bold, strikethrough na Italic kwa wakati mmoja utahitajika kutumia alama za unachohitaji katika kuanza neno lako na kuhitimisha.
Mfano, ukiandika “~bolditalics~” inafaa kutokea ikiwa bold-italics pamoja na strikethrough.
Mfano ujumbe wenye bold, italic na strikethrough
Je, umefanikiwa kuweza kufanya maandishi yawe bold, italic, strikethrough au vyote kwa pamoja?
WhatsApp waja na aina mpya ya Muandiko (font style)
Style za mwandiko ndani ya WhatsApp
Je haupendi aina ya mwandiko uliopo katika app ya WhatsApp? Usihofu, WhatsApp wapo njiani kuleta aina mpya ya muonekano wa herufi zake (font style) na muda wowote kuanzia sasa utaweza kuzitumia.
Maboresho haya yameshaonekana katika matoleo ya WhatsApp yaliyo katika matengenezo, yaani ‘Beta’.
Aina mbalimbali za mionekano ya herufi inayowezekana katika WhatsApp kwa sasa, mwishoni ndio muonekano wa ‘font’ mpya
Aina ya font utakayoweza tumia inafahamika kwa jina la FixedSys na unaiweza kuiona kupitia kompyuta yako ya Windows au ata kwa kutafuta Google.
Tatizo kuu ni jinsi ya kuitumia, inaonekana kama WhatsApp hawatatafuta njia rahisi kabisa ya font hiyo kutumika basi inawezekana wengi wakaona ni kazi kweli kuitumia mara kwa mara. Kuweza kutuma ujumbe katika muonekano huo inabidi unapoandika uweke alama tatu za kufungua na kufunga semi – mwanzoni na mwishoni…yaani ‘. Mfano – ”’UJUMBE WAKO”’
Kwa sasa uwezo huo upo katika toleo la beta, toleo namba 2.16.179 kwa Android na pia ata kwa iOS tayari lishaanza lishaanza kuonekana kwa watumiaji wa WhatsApp beta.
Ukiacha hili pia inasemekana WhatsApp wapo njiani kuleta uwezo wa kutumia video fupi za mfumo wa GIF na pia uwezo wa kupiga na kupokea simu katika mfumo wa video.
Gorilla Glass 5
Teknolojia Mpya ya Vioo Kufanya Simu yako Kuwa ngumu zaidi
Teknolojia ya vioo ya Gorilla Glass ndio teknolojia inayotumika zaidi katika ‘display’ za simu, tableti na vifaa vingine janja ili kuepusha kuvunjika pale vinapodondoka.
Muonekano wa kioo cha Gorilla Glass, kampuni ya Corning Inc inatengeneza teknolojia ya vioo hivi tokea mwaka 1962
Kampuni inayotengeneza vioo hivyo, Corning, imekuja na toleo jipya linalosemekana kuwa ni salama zaidi. Kampuni hiyo ya jijini New York nchini Marekani inadai vioo vyake hivi vipya vya Gorilla Glass vinanguvu ya zaidi ya mara nne ukilinganisha na vya wapinzani wake.
Inasemekana teknolojia ya Gorilla Glass inatumika katika zaidi ya vifaa bilioni 4.5 tokea mwaka 2007, wateja wakuu wa kampuni hiyo ya Corning ni pamoja Samsung, Apple, Motorola, LG, HP na makampuni mengine.
Gorilla Glass ndani ya majaribio
Inasemekana kwa toleo hili la 5 la Gorilla Glass basi uwezekano wa simu kutovunjika kioo pale ikidondoshwa kutoka umbali wa mabega au kiuno cha mtumiaji hadi chini unakuwa mkubwa sana..pia ni vigumu zaidi kioo kukwanguliwa na kitu.
Data kutoka utafiti mmoja wa kimataifa unaonesha ya kwamba takribani asilimia 85 ya watumiaji wa simu janja washaangusha simu janja zao angalau mara moja kwa kipindi cha mwaka mmoja….na asilimia 55 washaangusha kwa mara tatu au zaidi kwa kipindi hicho hicho.
Inategemewa muda si mrefu simu janja za hadhi ya juu kutoka makampuni makubwa zitakuja na toleo hili la kisasa la Gorilla Glass.
Je wewe unakubali ya kwamba kuvunjika kwa vioo vya simu ni moja kati ya tatizo kubwa zaidi kwa wamiliki wa simu janja? Unachukua hatua gani kuhakikisha simu yako inaendelea kuwa salama?
DTEK50: BlackBerry waja na Simu iliyo juu zaidi Kiusalama Duniani
Unapofikiria mwisho wa simu za BlackBerry umefikia ndio BlackBerry wanakuja na kitu kipya cha kukuonesha bado wapo katika biashara ya simu.
Simu hii mpya kutoka BlackBerry inayofahamika kwa jina la DTEK50 itaingia rasmi sokoni mwezi wa nane mwaka huu na kwa kiwango cha bei cha takribani dola za kimarekani 300 (t akribani Tsh Tsh 657,000/= | Ksh 30,400/= )
Nini kipya?
Hii ndio simu ya kwanza ya Android iliyo ya kugusa tuu(touchscreen) kutoka BlackBerry. BlackBerry ndio wanasifika zaidi duniani kwa kuwa na mifumo ya kiteknolojia salama zaidi ya kiusalama wa data dhidi ya udukuzi katika simu.
Na katika BlackBerry DTEK50 inaonekana wanaona kutumia Android ambayo tayari ni programu endeshaji maarufu zaidi ukichanganya na teknolojia za BlackBerry za usalama basi simu hii inaweza jipatia umaarufu kwa watu na mashirika yanayojali usalama wa data zao zaidi.
Simu hii ndiyo ilikuwa mwanzo inafahamika kwa jina la siri la BlackBerryNeon Sifa za kiundani
Kioo cha inchi 5.2 cha uwezo wa HD wa 1080p
Prosesa ya Snapdragon 617
Kiasi cha RAM cha GB 3
Diski Uhifadhi (storage) GB 16 huku ukiwa na uwezo wa kutumia memori kadi
Betri lisilo la kutolewa la mAh 2,610
Kamera ya selfi ya MP 8 huku ile kuu ikiwa ya MP 13.
Je itafanikiwa?
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya BlackBerry ameshashusha kiasi cha mauzo ya simu kwa mwaka ili biashara ya simu ionekane inaleta maana kwao. Mwanzoni wakati wanatambulisha simu janja ya BlackBerry Priv alisema ili wao waweze kuendelea na biashara ya utengenezaji simu basi ni lazima mauzo ya simu zao yawe si chini ya simu milioni 5 kwa mwaka…lakini sasa amebadilika na kusema mauzo yawe si chini ya simu milioni 3 kwa mwaka.
Kwa simu hii ambayo ata kibei ni nafuu kidogo ukilinganisha na zilizotangulia na hasa hasa ikionekana inavutia zaidi ata mashirika nyeti mpango huo wa kimauzo unaweza kufikiwa.
Saturday, July 23, 2016
Subscribe to:
Comments (Atom)








